Matthew 26:14-15

Yuda Akubali Kumsaliti Yesu

(Marko 14:10-11; Luka 22:3-6)

14 aKisha mmojawapo wa wale kumi na wawili, aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa viongozi wa makuhani 15 bna kuuliza, “Mtanipa nini nikimtia Yesu mikononi mwenu?” Wakamlipa vipande thelathini vya fedha.
Copyright information for SwhNEN